KATIBA YA VIJANA WA LONGOI

Mwongozo: Toleo la kwanza 2025

A. JINA LA KIKUNDI

Kikundi hiki kitajulikana kwa jina la UMOJA WA KUSAIDIANA LSS. Kitaanzishwa rasmi mnamo Septemba, 2025.

MADHUMUNI YA KIKUNDI

  1. Kusaidiana katika nyakati zote, za furaha na huzuni.
  2. Kuandaa matukio mbalimbali ya kijamii au kikundi yatakayotukutanisha pamoja kwa mwaka mara moja (kutoa misaada/charity, kutalii n.k).
  3. Kujitoa kwa hali na mali katika kuinuana kimaisha kwa kuunganishana na fursa mbalimbali na kuunga mkono kazi/biashara, huduma/bidhaa ya mwanakikundi.

B. UANACHAMA

Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama katika kikundi hiki iwapo ana sifa stahiki za kujiunga na kikundi kama zilivyoainishwa katika katiba hii.

SIFA ZA MWANACHAMA

NB: Kwa ujumla, mwanachama awe tayari kushiriki kazi za kikundi kwa kujitolea na kuhakikisha kuwa anakuwa na mchango mkubwa katika kukamilisha madhumuni ya kikundi hiki.

SIFA ZA MTU KUJIUNGA NA KIKUNDI HIKI

  1. Akubari kwa hiari yake kujiunga na kikundi.
  2. Awe tayari kuyaishi/kufuata maudhui sheria na kanuni zinazoongoza kikundi.
  3. Ajue kwamba kundi ni mali ya wanajumui ya Umoja wa Kusaidiana LSS.
  4. Pindi mwanachama mpya anapoungwa kwenye umoja huu atatakiwa kujitambulisha kwa utaratibu ufuatao:
    1. Majina matatu kamili
    2. Hali ya ndoa - ameoa/ameolewa
    3. Picha yako inayoonekana vizuri na makazi yake ya kudumu.

HAKI ZA MWANACHAMA

WAJIBU WA MWANACHAMA

UKOMO WA MWANACHAMA

Mwanachama atakoma uanachama ikiwa mambo yafuatayo yatatokea:

MICHANGO NA MASHARTI KWA MWANACHAMA

  1. Mwanachama aliyejitoa kundini kwa sababu za msingi kupoteza/kuibiwa simu, ubovu wa simu n.k ni wajibu wake kutafuta taarifa za maendeleo ya kundini bila kuathiri taratibu za kundi.
  2. Mwanachama yeyote mwenye lalamiko au hoja binafsi kuhusiana na maendeleo ya umoja wetu ni vyema akawasiliana na Kiongozi.
  3. Mwanachama yeyote atakaye patwa na tatizo au atakaye pata taarifa ya harusi inayomhusu mwanachama atalazimika kuwasiliana na uongozi na siyo kutoa taarifa hizo moja kwa moja ndani ya group.
  4. Mwenzetu akipatatwa na matatizo au harusi kwenye eneo husika kama yupo mwanachama tunaomba haende kuwakilisha.
  5. Lugha za matusi, kejeli na ugomvi, picha chafu, link zisizohusiana na kundi yaziruhusiwi. Ukikiuka unatolewa nje ya kundi kwa siku saba.
  6. Kila ifikapo tarehe 30 June na 31 Desemba ya kila mwaka, uongozi utaleta hoja kwa wanachama wa kundi ili kujadili na kufanya tathmini kama tumeenda vizuri wapi, tuboreshe nini, tuongezee au tupunguze. Mjadala huo utachukua siku 7 tangu hoja itolewe ili kumpa kila mwanachama nafasi ya kuchangia.
  7. Mwanachama atachangiwa pindi anapooa au kuolewa, atakapofiwa na Baba/Mama au Mlezi kwa mwanachama ambaye hana wazazi, pia Mtoto, Mume/Mke, na Wakwe au mwanachama mwenyewe anapofariki.
  8. Kiwango cha chini cha mchango kwa kila mwanachama ni 5,000/= kwa mwezi, mara moja. Isipokuwa kunapotokea dharura inayohitajika kutoa mchango wa ziada (magonjwa ya kufanyiwa oparetion pamoja na mtu kulazwa wodini kuanzia mwezi mmoja).
  9. Muda wa kuchanga:
    • Msiba: Siku 5 kuanzia tangazo la msiba.
    • Ugonjwa: Siku 7.
    • Harusi: Miezi 3 (siku 90) baada ya kupata taarifa.
  10. Mara baada ya kuanzishwa kwa umoja huu, kiingilio kwa mwanachama mpya ni 10,000/=.

NB: Kila aliyeridhia kuwa mwanachama wa umoja huu anapaswa kujiunga na M-KOBA (Bank mtandao) ambapo michango yote itakusanywa huko.

FAIDA ZA M-KOBA

  1. Inatunza taarifa zote za mwanachama.
  2. Inatunza taarifa za michango yote ya mwanachama, hivyo kurahisisha utolewaji wa huduma kwa mwanachama.
  3. Inatunza taarifa zote za fedha kwa uwazi na kuonyesha ujumbe wa aliyechangia, fedha inayoingia na inayotoka kwa wanachama wote.

UONGOZI

Kundi litakua na viongozi wafuatao:

UPATIKANAJI WA VIONGOZI

Viongozi wote watapatikana kwa kupigiwa kura na wanachama wote. Uchaguzi utafanyika kila baada ya miaka mitatu.

Fikia... wanachama wameshiriki

Jiunge na Umoja wa Kusaidiana LSS